TASAF 3 NA BeNKI YA DUNIA YAZIFIKIA KAYA MASKINI PEMBA_ZANZIBAR

Walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini shehia ya Shidi Wilaya ya Mkoani, wameuomba Ujumbe wa Benk ya dunia kuwaingiza katika mpango huo, baadhi ya wanakaya wenzao wenye maisha duni.

 Wamesema wamekuwa wakijisikia tabua, wakati wanapokuwa wanapokea fedha zinazotolewa na TASAF III, huku baadhi ya wenzao wakishindwa kupata ruzuku hiyo.
Wanakaya wa shehia ya shidi wameeleza hayo, katika mkutano wa maalumu ya wajumbe wa benk ya dunia na Uongozi wa TASAF walipokuwa katika ziara ya siku mbili Kisiwani Pemba.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa mfuko wa TASAE Ladislaus Mwamanga, amesema shehia ya shidi ni miongoni mwa vijiji na shehia 10 Tanzania zilizotembelewa na Ujumbe wa benk ya Dunia, kutokana na utekelezaji mzuri wa kazi katika vijiji Elfu 10, Tanzania nzima 












Previous
Next Post »

Ads