Wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki wakiwa nje ya Jengo la Baraza
Mkutano wa pili wa jumuiya ya bunge la afrika mashariki unatarajiwa kuanza leo ambapo rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa baraza la mapinduzi dkt Alli Muhammed shein anatarajiwa kufungua mkutano huo,nae spika wa bunge hilo Daniel kidega amesema mambo mbali mbali yatajadiliwa katika kikao hicho ikiwemo kupitishwa kwa miswaada.
Akizungumza na Mbwanajr nje ya mkutano huo mbunge wa bunge hilo Mariam Yahya amesema miongoni mwa miswada ambayo itawasilishwa wa kuzuia kutumia mifuko ya plastic mswaada kusafirisha binaadamu kinyume na sheria na mmswada wa kijinisa ambao utakaoweza kuleta usawa katika jamii.
Jumla ya miswada mitatu inatarajiwa kujadiliwa kuanzia leo katika ukumbi wa baraza la wawakilishi chukwani ambapo itahusisha wabunge kutoka nchi za afrika mashariki ikiwemo Tanzania ,Burundi ,Kenya na uganda
ConversionConversion EmoticonEmoticon