Zanzibar kuondoa ukosefu wa dawa hospitalini

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya imesema itahakikisha inaondowa tatizo la ukosefu wa dawa katika hospitali zote zilizopo kwa lengo la kurahisisha huduma hiyo kwa wananchi wanaofuata matibabu.




   Mkurugenzi wa Bohari kuu ya dawa Zanzibar Zahran Ali Hamada amesema Serikali tayari imeidhinisha  shilingi bilioni 1.6 kwa ajili ya kununulia dawa na na kusambaza mahospitalini.

   Hata hivyo amesema katika mwaka wa fedha 2016/17 Serikali imetenga shilingi bilioni tano kwa ajili ya kununulia dawa ambazo zinakidhi  mahitaji ya wananchi katika kuendeleza azma ya Serikali ya kutoa huduma za afya kwa wananchi bila malipo.

 
   Aidha amesema wizara itaandaa utaratibu wa kufuatilia matumizi ya dawa hizo ili kuhakikisha zinawafikia wananchi kwa wakati bila kupata usumbufu unaojitokeza.

   Kwa upande wake Daktari Msaidizi wa Hospitali ya Makunduchi Dkt.  Asha Salum Hassan amesema hali ya dawa hivi sasa inaridhisha na dawa nyingi muhimu zinapatikana isipokuwa dawa za maumivu na Anti biotic zinatumika kwa wingi hospitalini hapo.



Previous
Next Post »

Ads