Makamu wa rais wa cuba kuwasili leo Zanzibar

Salvador Antonia Messa
 Makamu wa rais wa Cuba Salvador Antonia Messa anatarajiwa kuwasili zanzibar leo jioni kwa ziara ya siku mbili ya kiserikali.
Taarifa iliyotolewa na waziri wa nchi afisi ya makumu wa pili wa rais Mohammed Aboud Messa atapokelwa na mwenyeji wake makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd katika uwanja wandege wa Zanzibar.
Akiwa nchini atafanya mazungumzo na rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Sheini na baadae kufanya mazungunzo na makamu wa pili wa rais balozi Idd.
Cuba ni miongoni mwa nchi zinazoisaidia Zanzibar hasa katika sekta afya ambapo nchi hiyo imechukua jukumu la kuwasomesha vijana kadhaa katika fani ya udaktari wa bindamau.
Hapa akiwa na makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Samia Hassan Suluhu

Previous
Next Post »

Ads