Waziri wa kilimo mali asili mifugo na uvuvi Zanzibar Hamad Rashid
amewataka wakulima wa kilimo cha mbogamboga na matunda kujiunga na vikundi vya
ushirika ili kunufaika na huduma ya mikopo inayotolewa kwa lengo la kuboresha
maendeleo katika kilimo wanchozalisha.
Akizungumza na mbwanajr huko ofisini kwake
maruhubi amesema wafanya biashara wengi wakiwemo wakulima wa mbogamboga wanafanya
biashara kinyume na utaratibu jambo ambalo linapekekea kutotambuliwa kisheria
na kukuso huduma ya kupatiwa mikopo.
Hata hivyo
amesema wakulima wanapojikusanya pamoja na kubuni njia bora za kuimarisha
maendeleo ya kilimo itarahisisha upatikanaji wa kupatia mikopo kwa wakati na
kuingia katika kilimo cha biahara kwa lengo la kujikombowa na umaskini na
kukuza uchumi wa nchi.
Aidha ametowa wito kwa wakulima kuzitumia
taasisi za fedha katika shughuli zao za kilimo ili kurahisisha kutambuliwa
kisheria wakati wa kupatiwa mahitaji muhimu kazi kazi zao.
Zaidi vikundi kumi na sita ikiwemo zimepatiwa
mikopo ya kujiendeleza na kilimo ili kufikia kilimo cha bishara.
ConversionConversion EmoticonEmoticon