Mamlaka ya
mapato Tanzania TRA Zanzibar imesema imebadili mfumo wake wa sasa wa
kuhifadhi kumbu kumbu za walipa kodi na kuweka mfumo wa kisasa unaoendana na
ukuaji wa teknolojia.
![]() |
| Saleh Haji Pandu |
Akizungumza na mwanahabari
wetu afisa elimu kwa mlipa kodi wa mamlaka hiyo Saleh Haji Pandu amesema wameamua
kuandaa mkakati maalum kwa wafanya biashara na kuhakiki taarifa zao kwa kumjua mlipa kodi yupo maeneo
Fulani anayofanyia biashara.
Amesema ni vyema kwa wafanya biashara wenye TIN kuboresha au kuhakiki taarifa katika ofisi za mkoa na wenye TIN zisizo za biashara kuhakiki taarifa
zao katika ofisi yoyote ya TRA.
Akizungumzia ongezeko la watu wanaofanya biashara katika
maeneo yasiyokuwa rasmi na kutolipa kodi,amesema hali hiyo inaipa mzigo Serikali
katika kuendesha huduma za jamii na kutotimiza lengo walilokusudia.
Aidha ameitaka jamii kuwa na uzalendo wa kusajili biasha
zao ili kuona mamlaka hiyo inafikia lengo hasa la kufanikisha matarajio yao ya
kuwepo kwao na kuwata wananchi kudai risiti.




ConversionConversion EmoticonEmoticon