SHIRIKA la Shina Inc la nchini Marekani na Tanzania,limetambulisha blanketi la kuulia wadudu wasumbufu na wale wanaosambaza maradhi kama mbu, chawa na kunguni.
Katika utambulisho huo, rais wa shirika hilo nchini Marekani na Tanzania, Jesca Mushala alisema kuwa kama mtanzania akiwa nje ya nchi yake aliona kitu hicho kuwa ni kizuri ndio maana akafanya jitihada ili kiweze kuwasaidia watanzania waishio kwenye maeneo yenye wadudu hao hususani mbu.
alisema mablanketi hayo yamethibitishwa kwa majaribio mbalimbali kuwa ni salama kwa binadam, hivyo kwa hapa nchini wamekuja na blanketi 1100 kwa ajili ya kusambaza na majaribio kwa hapa ili tupate pia maoni kutoka kwa watumiaji.
Alisema hapa nchini wameanzia mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Kagera, Pemba na Unguja na baada ya hapo wataangalia mrejesho watakaoupata kabla ya kusambaza nchi nzima.
Aliongeza kuwa juu ya blanketi hilo mbu hawezi kuruka juu ya futi tano kwenye blanketi hilo.matumizi yake ni kujifunikia wakati wa kulala ama ukiwa unatembea.
Blanketi hilo lina teknolojia ya kisasa, utafiti wake umefanywa kwa miaka 25 na zinatumika kwa nchi 40 duniani.
| wanakikundi cha sanaa hawakuwa nyuma kuelimisha |

ConversionConversion EmoticonEmoticon