VIJANA WAPANGIWA MIKAKATI ZANZIBAR


Mwenyekiti wa baraza la vijana taifa Khamis Rashid Kheri amesema katika uongozi wake mpya atahakikisha vijana wanashirikiana pamoja katika harakati za kujikwamua kichumi
Akizungumza na waandishi wa habari mjni Zanzibar amesema lengo la kuundwa baraza hilo ni kuona vijana wanaondokana na dhana  ya utegemezi hasa katika masuala ya uchumi.
Nae makamu mwenyekiti wa baraza hilo Maryam Mwishau Abdallah amesema baraza hilo litajitahidi kupunguza wimbi kubwa la utumiaji wa dawa za  kulevya linalowakabili vijana nchini.
          Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imeshauriwa kujenga gereza la watoto ili kuondoa tatizo liliopo la kuwachanga watoto hao na mahabusu wakubwa.
Akiuliza swala katika baraza la wawakilishi mwakilishi wa jimbo la Mpendae Saidi Mohamed Dimwa amesema kuwachanganya watoto na mahabusu kwenye gereza moja kutawafanya kuiga mambo ya wakubwa.
 Nae waziri wa nchi ofisi ya rais tawala za mitaa na vikosi maalum vya SMZ Haji Omar Kheir amesema kwa mwaka huu wa fedha serikjali imetenga shilingi milioni 250 za ujenzi wa gereza la watoto Hanyegwa mchana Wilaya ya Kati.
Amesema kati ya fedha hizo mwezi huu serikali imetoa shilingi milioni 100 kwa ajili ya ujenzi wa gereza hilo.
Aidha waziri Kheir amesema kwa sasa serikali imewatenganisha wafungwa watoto na watu wazima kwenye gereza la Kilimani, Wilaya ya mjini chini ya ufadhili wa shirikal la kuhudumiwa watoto UNICEF.
         Wauguzi 27 wa hospitali kuu ya Mnazi Mmoja wamepewa onyo baada ya kuiacha maiti ya mtoto mchanga kwenye wodi ya wazazi kwa muda wa siku tatu.
        Akijibu suala katika kikao cha baraza la wawakilishi waziri wa afya Mahamoud Thabit Kombo amesema onyo hilo limetolewa kufuatia waguzi hao kushindwa kutekeleza kanuni inayowataka mtu anaekufa kama hajatokea wenyewe kupeleka chumba cha kuhifadhia maiti ‘Mortuary’.
        Amesema uchunguzi uliofanywa umegundua mzazi alielazwa alikuwa hali mbaya, lakini mumewe alietakiwa kununua baadhi ya vifaa na kuacha namba za simu hakufanya hivyo.
        Hata hivyo amesema kosa hilo ni la pande mbili kati ya wazazi kushindwa kudai maiti yao na wauguzi wa shifti tatu za wodi hiyo kuiacha maiti hiyo wodini kwa siku tatu.
Tukio hilo limetokea tarehe 18 July mwaka huu baada ya mama huyo mjamzito alieletwa kujifungua kwa njia ya upasuwaji akitokea hospitali ya Mwembeladu.
     Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni  na Michezo Zanzibar imesema  imeshazibiti na kutafutia ufumbuzi baadhi ya changamoto zilizokuwa  zikikwamisha upatikanaji  wa idadi sahihi  za wageni wanaoingia nchini.
     Akijibu swali  kwa wajumbe wa baraza la wawakilishi Naibu waziri Chum Khamis Kombo amesema upatikanaji wa idadi sahihi za wageni  umeweza kusaidia   na  kuhakikisha kuwa hakuna  uvujaji wa mapato katika sekta ya utalii kwa kutumia njia ya ukaguzi  katika miradi ya utalii kwa ajili ya kuhakikisha wawekezaji wanalipa kodi,kuwashajihisha wafanyabiashara kufanya malipo kupitia benki na  kuwawezesha wajasiriamali katika sekta ya utalii ili waweze kutoa huduma bora kwa wageni.
       Zaidi ya asilimia 80  ya fedha za kigeni linachagia katika ukuwaji wa pato katika sekta ya utalii hapa Zanzibar 
Previous
Next Post »

Ads