Tunda Man ‘asiyepata kadi anione’

Mkali wa wimbo ‘Mama Kijacho’ Tunda Man amesema tarehe 12 mwezi Novemba atafunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu.
Tunda amesema kuwa ndoa hiyo ilikuwa ifanyike miezi michache iliyopita lakini amedai kuna mambo yaliingilia na kuharibu mipango ya ndoa hiyo.
“Kusema kweli suala la kuoa, naoa mwezi wa kumi na moja tarehe 12,” alisema Tunda “Kwa hiyo mtu yeyote anakaribishwa na nipo tayari kuingia kwenye maisha ya ndoa. Kwa wale ambao hawajapata kadi wanione, unajua kuna watu mpaka waalikwe ndo wanaweza kuja,”
Muimbaji huyo amesema anaimani akiingia kwenye ndoa kuna neema ambayo ataipata kutoka kwa mwenyezi mungu.
Previous
Next Post »

Ads