Ni ukweli usiopingika kuwa kwa sasa muziki wa Tanzania umepata tobo ambalo kwa muda mrefu ulikuwa ukilitafuta ili uweze kupenya nje ya nchi nyingine – hilo limefanikiwa kwa sasa.

Msanii wa muziki wa Dance Hall hapa Bongo, Chibwa amefanikiwa kupata bahati ya kuwa msanii pekee kutoka Tanzania kuchaguliwa na kupatiwa beat ambalo limetumiwa na wasanii wa nchi nyingine duniani (Riddim) ikiwemo Jamaica, Afrika Kusini, Canada, Ghana, Kenya na Zimbambwe ambapo nyimbo hizo zimeingizwa kwenye albamu ya pamoja iliyopewa jina la ‘Pharaoh Riddim’.
Beat la wimbo huo limetengenezwa na mtayarishaji wa muziki kutoka Afrika Kusini Dj Wallas akishirikiana na Bashment Sound ya nchini humo na kuwapatia wasanii waliotengeneza nyimbo hizo akiwemo Wyre (Kenya), NC Dread (Afrika Kusini), Mavluz & Sheggy Styla (Ghana), Miz Dee (Zimbabwe), Dudsymil (Canada) na Bay C (Jamaica).
Akiongea na kituo kimoja cha redio leo Chibwa amesema kuwa ni bahati kubwa kwake kwa kuwa hapa Bongo wasanii wengi wanafanya muziki lakini yeye ndiye aliyechaguliwa kufanya hivyo.
“Ni kama bahati kwangu na kitu cha heshima pia. Wasanii hapa Bongo tupo wengi lakini nimeweza kuonekana mimi, hiyo inaonyesha ni jinsi gani nazidi kupiga hatua. Ukweli muziki wa Bongo kwa sasa umefika mbali,” amesema Chibwa. Kwa upande wake Chibwa ametumia beat hilo kutengeneza wimbo alioupa jina ‘More Ting’

ConversionConversion EmoticonEmoticon