Rais Magufuli atema cheche uzinduzi wa Ndege Mpya za Air Tanzania


Rais DKT JOHN MAGUFULI amelitaka shirika la ndege nchini ATCL kubadilika na kufanyakazi kwa weledi ili kumudu ushindani
Rais DKT JOHN MAGUFULI amelitaka shirika la ndege nchini ATCL kubadilika na kufanyakazi kwa weledi ili kumudu ushindani katika kutoa huduma ya usafiri wa anga nchini.

Rais MAGUFULI ametoa kauli hiyo jijini DSM wakati wa uzinduzi wa ndege mpya zilizonunuliwa na serikali kwa lengo la kuboresha usafiri wa anga nchini ambapo amewataka watendaji wa shirika hilo kuzitumia ndege hizo kwa manufaa ya taifa zima na kumudu ushindani wa kibiashara katika usafiri wa anga.

Pia Rais MAGUFULI amesema serikali inatarajia kununua ndege zingine mbili kubwa zenye uwezo wa kubeba abiria mia moja sitini na nyengine yenye kubeba abiria mia mbili na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya usafiri wa anga.

Katika hafla ya uzinduzi wa ndege hizo zilizofanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Julias Kambarage Nyerere, Rais MAGUFULI amesema ndege hizo zina ubora unaokubalika na zenye kumudu mazingira ya viwanja vingi vya ndege hapa nchini.



Previous
Next Post »

Ads