Naibu Katibu wa
wizara ya kilimo mali asili mifugo na uvuvi Zanzibar Dokta Islam Seif
Salum Amesema takwimu zinaonesha kuwa idadi ya watu wasiopungua hamsini na tisa elfu wanakufa kila mwaaka
duniani kote kutokana na ugonjwa wa kicha cha mbwa.
Akizungumza katika uzinduzi wa siku ya kichaa cha
mbwa dunia wenye lengo la kuhamasisha wafugaji pamoja na kutoa
elimu kwa ajili ya kuchanja ili kuweza
kupunguza athari za kifo zitokanazo na ugonjwa wa kichaa cha mbwa huko Chaani Kubwa wilaya ya kaskazini A Unguja.amesema
hli hiyo ikiendelea itapelekea vifo vya watu wasiopungua laki nane na thamanini
na tano u elfu ifikapo mwaka 2030
Kwa upande wake doktari mkuu wa mifugo Waridi Abdallah
Mussa Akitoa taarifa ya ungonjwa huo amesema hapo mwanzo ugonjwa huo ulikua
haupo lakini uliongezeka kwa sababu tafauti zikiwemo kwa baadhi ya wafugaji
kuingiza wmifugo kutoka maeneo mengine ya nje ya Zanzibar
Nae sheha wa shehia ya Chaani Kubwa Abdul Ghafar Ibrahim Ussi amesema katika kijiji cha Chaani kuna wafugaji
wengi wa mbwa lakini anafurahishwa na wafugaji hao kuwa ana mwamko wa
kujitokeza kupatiwa huduma hizo.
Maadhimisho hayo huaadhiumishwa kila ifikapo tarehe 28
mwezi Spetembar ya kila mwaka duniani Zaidi ya mbwa mia mbili wanatarajia
kupatiwa chanjo za magonjwa mbalimbali kijijini hapo..





ConversionConversion EmoticonEmoticon