Wikii hii imekuwa mbaya kwa mchezaji wa timu ya Barcelona baada ya kupasuka na kutoka damu wakati wa mechi za kuwania kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2018 wakati timu ya Brazil ilipokuwa ikicheza na Bolivia.
Brazil walikuwa nyumbani kwenye uwanja wao wa Arena das Dunas na walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 5-0. Magoli hayo yalifungwa na Neymar, Phillip Coutinho, Filipe Luis, Gabriel Jesus na Robert Firmino.
Kwenye mchezo huo Neymar alilazimika kutoka nje ya uwanja kwenye dakika ya 68 na nafasi yake kuchukuliwa na mchezaji wa Chelsea, William baada ya kupigwa kiwiko usoni na beki wa Bolivia, Ronaldo Raldes hadi kupasuka.
Hapa chini la tukio hilo.






ConversionConversion EmoticonEmoticon