Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) Leo ratiba

Ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea leo Oktoba 7, 2016 kwa michezo miwili ambako Kagera Sugar itaikaribisha Toto Africans kwenye Uwanja Kaitaba mkoani Kagera wakati Stand United itakuwa mgeni wa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
football
Mechi zingine zitapigwa kesho, Jumamosi Oktoba 8, 2016 pia kutakuwa na michezo mitatu ambako Majimaji ya Songea itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea wakati African Lyon itaikaribisha Ndanda FC jijini Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikiialika Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi ulioko mkoani Pwani.

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia kwa ku like FacebookTwitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga naYoutube kuangalia video zote kali kutoka mbwanajr !

Previous
Next Post »

Ads