Wakaazi wa fuoni na watumiaji wa barabara hiyo wameishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuweka alama za usalama wa barabarani mara baada yakumazika kwake ili kuepukana na ajali zinazosababishwa na madereva wanaoendesha vyombo kwa kasi.
Wakizungumza na mwandishi wetukwa nyakati tofauti baadhi ya wakaazi hao Muhammed Mbaruk na Iddi Ali wamesema wameridhishwa na ujenzi wa Barabara hiyo lakini wanawasi wasi mkubwa juu kwa kuchelewa kumalizika kwa wakati ili kuwekwa na alama za kisalama.
Aidha wamesema baadhi ya madereva wanaendesha vyombo vya moto kinyume na utaratibu hivyo ni vyema kwa serikali kusimamia ipasavyo ujenzi unaoendelea kwa lengo la kuondoa matatizo yanayowakabili watumiaji na wakaazi wa barabara hiyo ikiwemo ajali za mara kwa mara.
Barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 4 imeaza matengenezo tangu novemb11 mwaka jana chini ya usimamzi wa kampuni.


ConversionConversion EmoticonEmoticon