Ofisi ya Kuratibu Misaada ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imetoa ripoti kuwa, kimbunga Matthew kilichoikumba Haiti kimewaathiri watu milioni 1.3. Miongoni mwao, watu laki 7.5 wanahitaji msaada wa dharura.
Ripoti hiyo imesema, nyumba zaidi ya laki 2 zimeharibika. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP pia limesema, asilimia 80 ya mazao katika sehemu ya kusini mwa Haiti ambayo imeathirika vibaya zaidi, yameharibika.
Hivi sasa, kutokana na hali mbaya ya hewa na kushindwa kupitika kwa barabara, idadi halisi ya vifo kwenye maafa hayo itatangazwa baada ya siku nne tano.

ConversionConversion EmoticonEmoticon