Wakati huo huo inafahamika kuwa, Ukad pia linachunguza tuhuma katika jarida la Daily Mail Uingereza kuwa kifurushi cha dawa kiliwasilishwa kwa timu ya Sky na kocha mmoja wa Uingereza nchini Ufaransa 2011.
Inadaiwa kuwa kifurushi hicho kiliwasilishwa Juni 12, 2011, siku ambapo Muingereza Sir Bradley Wiggins alishinda mashindano ya Criterium du Dauphine huko La Toussuire.
Timu Sky imesema imefanya kaguzi wa ndani na ina imani kuwa "hakuna makosa yaliofanywa".
"tumewasiliana na taasisi ya kitaifa ya uendehsaji baiskeli nchini kuhusu tuhuma hizo na tumeiomba iwasiliane na Ukad, ambalo litaendelea kushauriana nayo," imesema timu Sky.
Msemaji wa Ukad amesema: "shirika la kupambana na matumizi ya madawa ya kutitimua misuli Uingireza inachunguza tuhuma za makosa katika uendeshaji baiskeli. Katika kulinda hadhi ya uchunguzi hatuto toa kauli ya ziada."


ConversionConversion EmoticonEmoticon