October 8 2016 mechi za kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia 2018 Urusi kwa mataifa ya Ulaya ziliendelea kama kawaida, October 8 inapigwa michezo tisa kama ilivyopigwa October 7 2016, timu ya taifa ya England yenyewe ilikuwa mwenyeji wa timu ya taifa ya Malta katika dimba la Wembley London.
Mchezo kati ya timu ya taifa ya England dhidi ya Malta uliandika historia mpya kwa kinda wa Man United Jesse Lingard ambaye alipata nafasi ya kuichezea timu ya taifa ya England ya wakubwa kwa mara ya kwanza katika maisha yake ya soka.
Katika mchezo huo England walikuwa wenyeji na walionesha hali ya kumiliki mpira kwa asilimia 77 kwa 23 dhidi ya Malta, kitu ambacho kiliwafanya waibuke na ushindi wa goli 2-0, zilizofungwa na mshambuliaji wa Liverpool Daniel Sturridge dakika ya 29 na nyota waTottenham Hotspur Dele Alli dakika ya 38.
ConversionConversion EmoticonEmoticon