Cristiano Ronaldo akiifungia bao la kwanza Ureno dakika ya 68 katika ushindi wa 6-0 dhidi ya Andorra kwenye mchezo wa Kundi B kufuzu Kombe la Dunia usiku wa jana Uwanja wa Manispaaa wa Aveiro mjini Aveiro. Ronaldo alifunga mabao manne jana mengine dakika za pili (2), nne (4) na 47. Katika mchezo huo ambao wachezaji wawili wa Andorra, Jordi Rubio dakika ya 62 na Marc Rebes dakika ya 70 walitolewa kwa kadi nyekundu kwa kumhezea rafu Ronaldo, mabao mengine ya Ureno yalifungwa na Joao Cancelo dakika ya 44 na Andre Silva dakika ya 86 picha chini hapo
|
ConversionConversion EmoticonEmoticon