Ufisadi Nigeria: Majaji wanaswa na $800,000 nyumbani

Rais Buhari akiwasalimia baadhi ya wakuu wa polisi
Mamlaka kuu inasema kwamba imenasa zaidi ya dola elfu 800,000 katika sarafu tofauti pale ilipotekeleza uvamizi wa ghafla wa vita dhidi ya ufisadi, miongoni mwa majaji kadha waandamizi.
Pesa hizo zilizokuwa katika sarafu za Nigeria na kigeni, zilipatikana nyumbani kwa majaji hao ambao bado hawajatambuliwa.
Rais Muhammadu Buhari alizindua vita vikali dhidi ya ufisadi, huku akisema kuwa mabilioni ya dola yaliibwa muda mfupi kabla hajaingia mamlakani mwaka jana.
Lakini wakosoaji wake wanamlaumu kwa kuwalenga wapinzani wake wa kisiasa.
Previous
Next Post »

Ads