Serikali yavunja Misingi ya nyumba Magharib A



Seriakli ya wilaya ya magharib A imechukua hatua ya kuwavunjia  watu misingi ya nyumba wanaojenga aktika ameneo yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo katika eneo la Mfenesini selem.
Baadhi ya wananchi wakitoa hisia zao baada ya zoezi hilo kukamilika wamesema wameridhishwa na hatua iliyochulkuliwa na seriakli ya mkoa huo kutokana na maeneo hayo kuavmiwa na baadhi ay watu ambayo hapo awali walikua wanatumia kwa shughuli za kilimo na kupelekea kuharibiwa kwa vipando vyao.


 Nae kaimu wa mkurugenzi manispaa ya magahrib A Ali Abdallah Natepe amesema  hatua hiyo imekuja kutokana na ukaidi wa wananchi wenyewe kuamua kufanya shughuli za ujenzi katika eneo  hilo 

Mkuu wa wilaya hiyo Mwinyiusi Abdallah Hassan amesema eneo hilo lipo katika kazi za kilimo lakin anasikitishwa na baadhi ya wananachi kupinga agizo hilo  nakusema bado baadhi ya wananchi hawataki kutii sheria bila ya shuruti.

Hata hivyo amesema tatizo hilo lipo katika maeneo mbalimbali ya baraza la manispaa ya  magharib A akiyajata baadhi ya ameneo ambayo yatawajibika kwa kuvunjwa kutokana na sababu tafauti  ni Kinuni, Chuwini katika shamba la Serikali, mgeni hendi, shelikia jiwe fusi.Aidha amewataka wananchi wafate taratibu zote za sheria kabla wanapoamua kutaka kujenga  nakuacha kuchukua sheria mikononi .


Mkuu wa mkoa mjini magharib Ayuob Muhammed Mahmoud amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itachukua hatua ya kuyazibiti  maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya mpango maalumu kwa kuwavunjia watu waliojenga katika maeneo   hayo.

 Akizungumza na waandishi wa habri  kuhusu uendelezaji wa miradi ya mAendeleo  inayotekelezwa katika mkoa wa mjini magharib  katika vijiji vya Fumba na nyamazi Dimani hapo Ofisini kwake vuga amesema serikali haiku yachukua maeneo yote ambayo yamepangwa katika mpango maaalum imejaribu kuangalia eneo lilitengwa maalumu kwa ajili ya watu wa funya kazi za ujenzi.

Akifafaua kuhusu uimarishaji wa eneo la darajani  mkuu wa mkoa amesema  seriakli inaendelea na maandalizi na hapo baadae taaasisi husika itatoa taarifa maalumu kuhus kuanza kwa ujenzi katika eneo hilo.


Previous
Next Post »

Ads