Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Mbwana Samatta jana amepokea habari nzuri iliyotangazwa na shirikisho la soka Afrika CAF, good news ya Samatta iliyopokelewa na watanzania ni kutokana na kutajwa katika list ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2016.
Mtanzania Mbwana Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2015 kwa wachezaji wanaocheza Ligi za ndani ya Afrika, safari hii amepata nafasi ya kuwania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla kwa mara ya kwanza akiichezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.
ConversionConversion EmoticonEmoticon