MOBILE COURT YAANZA KUFANYA KAZI WILAYANI TUNDURU


Mkuu wa wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma Mhe. Juma Zuberi Homera amefanya mkutano wa hadhara wenye lengo la kusikiliza kero za wananchi katika kata ya mbati wilayani humo.
Mhe. Homera aliongozana na kamati yake ya Ulinzi na Usalama, Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Tunduru pamoja na Hakimu na karani wa Mahakama ya mwanzo Tunduru.
Mkutano huo wa hadhara ulianza kwa wananchi kutoa kero zao mbele ya Mkuu wa wilaya, akitoa dukuduku lake ndugu Ali Rashid alisema "Serikali imekuwa ikiwaagiza wananchi kuanzisha vikundi vya maendeleo lakini cha ajabu hawajawai kupata hata senti".

Nae ndugu Mohammed Issa alisema " nakushukuru Dc Homera kwa kutupa nafasi ya kutusikiliza sisi wananchi wa kawaida, jambo linalo nisumbua ni huyu mtendaji wa kijiji, tulimpa mchango wa madawati zaidi ya shilingi milioni moja ila sisi wananchi hatujui fedha hizo zimekwenda wapi?".
Mhe. Homera akijibu maswali hayo, aliwahasa wananchi kuwa na imani na serikali ya awamu ya tano "muda wa siasa umekwisha sasa ni kazi tu, nawaomba mtuoneshe ushirikiano swala la kuunda vikundi nawahasa muendele kuunda na vikundi vilivyopo viendelezeni, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameshatenga fedha za milioni 50 kwa kila kijiji na hela hizo wananchi mtapata kupitia vikundi lakini kuna hela halmashauri ya asilimia 5 kwa vijana na wakina mama namuagiza mkurugenzi ahakikishe hili linatekelezwa kwenye bajeti hii 2016/17".
Dc Homera akimwelezea Mtendaji wa kijiji anayeshutumiwa kwa kula zaidi ya shilingi milioni moja alisema "najua huyu mtendaji aliomba likizo ili wananchi wasahau hili swala, namuagiza popote alipo anitafute ndani ya siku 3 na watu wangu nawaagiza wafuatilie hili swala na ndani ya siku 3 nataka majibu".
Katika kata ya mbati kuna mgogoro wa ardhi kati ya kijiji cha mbati na mdabwa na wananchi wanatumia sana pombe haramu aina ya gongo, Mkuu wa wilaya aliagiza viongozi wa vijiji vinavyo kinzana kwenda halmashauri kitengo cha ardhi na kuoneshwa mipaka yao na atakaye endeleza mgogoro huo atachukuliwa hatua na kuhusu gongo aliwaagiza wananchi kutoa taarifa ya watu wanao tengeneza na kuuza popote wanapo pata taarifa watoe kwa jeshi la polisi na alitoa namba ya Mkuu wa kituo(OCS) 0789 709 370 na ya Mkuu wa Upelelezi(OC-CID) 0659 884 800.

Mkuu wa wilaya alimuagiza hakimu kuwafungulia na kuwasomea mashitaka watuhumiwa wote ambao watoto wao hawajaenda shule wakati walifaulu na wale wanafunzi watoro.
Wanafunzi ambao ni watoro walio wengi wanatumikishwa kazi za shambani, wengine waliondolewa shuleni Kwa kupata ujauzito, wengine wamekuwa wakitoka mashuleni nakujishughulisha na shughuli mbali mbali za ujasiliamali na walio wengi hufanya kazi kwenye makampuni ya ujenzi wa barabara, tangu mradi wa barabara ya Tunduru Mangaka hadi Namtumbo kuanza.
Jumla ya wanafunzi walio chukuliwa hatua kufikia 12 kutoka sekondari ya kutwa ya Marumba ambayo Kwa mfano wanaotarajia kuhitimu mwaka 2016 walianza kidato cha kwanza 64 mwaka 2013 na wanatarajia kuhitimu wanafunzi kidato cha nne 17 akiwemo msichana mmoja tu na shule ya secondary Mchoteka walianza shule wanafunzi 100 mwaka 2013 na wanatarajia kuhitimu wanafunzi 21tu.
Watu wawili walichukuliwa hatua ni Bw. Jimmy Bandawe ambae ni Afisa mtendaji wa kijiji cha Mpanji na mwanae anaitwa Farida Jimmy na Bw. Hamis Mjeje toka kijiji cha Mdaba na mwanae Majid Hamis.
Hukumu zilizotolewa jana na watu 5 wamepelekwa gerezani kwa kushindwa kulipa faini ya 200,000 na kwenda jela miezi miwili lakini wakitoka watatakiwa kufyatua matofali 2000 kila mmoja na watu 7 wali hukumiwa kifungo cha nje miezi miwili na kufyatua matofali 2000, hukumu hii ilitolewa kwa wale wasiojiweza wazee na wagonjwa.
Vilevile Mhe. Juma Zuberi Homera alitaka kuwa weka ndani Mwenyekiti wa kijiji cha Mdabwa Bw. Said White na Mwenyekiti wa kitongoji cha kawawa Bw. Issa Hassan kwa kosa la kukaidi agizo la serikali la kufyatua matofali 100,000 kwa kila kijiji ila DC alitumia busara ya kuwaacha kwa sharti la kuanza kufyatua matofali hayo mapema iwezekanavyo.

CREDIT:DC HOMERA TUNDURU
Previous
Next Post »

Ads