Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Libya amelaani mashambulizi yaliyofanywa katika majengo ya serikali Mjini Tripoli mji mkuu wa Libya.
Martin Kobler amelaani shambulio lililotekelezwa katika moja ya majengo ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya katika mji mkuu Tripoli na kutahadharisha kuhusu kushtadi machafuko nchini humo.
Aidha, Kobler ameongeza kuwa pande zote za Walibya zinapasa kuacha kuzusha mivutano ili kudhamini maslahi ya nchi hiyo.
Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Katika Masuala ya Libya pia amezitaka pande zote za kisiasa zenye ushawishi nchini humo zishirikiane na Baraza la Uongozi la serikali ya Umoja wa Kitaifa ya nchi hiyo.
Kobler amekumbusha kuwa Baraza la Uongozi la Libya ni taasisi pekee ya kisheria nchini Libya kwa mujibu wa makubaliano ya kisiasa ya nchi hiyo yaliyofikiwa katika mji wa Sakhirat nchini Morocco.
Itakumbukwa kuwa, Khalifa al Ghawil Mkuu wa serikali ya zamani ya Libya ambayo ilikuwa na makao yake huko Tripoli; serikali ambayo ilikuwa ikijiita serikali ya ukombozi wa kitaifa, Ijumaa iliyopita akiwa katika majengo muhimu ya serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya alitangaza kuwa, serikali hiyo ya huko nyuma imechukua madaraka.
Khalifa al Ghawil Mkuu wa serikali ya zamani ya Libya iliyokuwa na makao yake Tripoli.
ConversionConversion EmoticonEmoticon