Mchezaji wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani, Shkodran Mustafi amezungumzia umuhimu wake wa kuwa na imani ya dini ya Kiislamu.

Nyota huyo mwenye asili ya Albania, ambaye anacheza nafasi ya beki wa kati na pembeni mwenye umri wa miaka 24 hivi karibuni alifanya mahojiano na gazeti la The Sun na kubainisha umuhimu wa kuwa na imani ya dini ya Kiislamu.
Alisema nia yake ya kutaka kutekeleza ibada ya Hijjah, akisema, “Uislamu ni muhimu kwangu kuliko kila kitu.”
Mustafi pia alisema hupata ugumu wakati mwingine katika jitihada za utekelezaji wa baadhi ya ibada za Kiislamu hasa katika mwezi mtukufu wa Ramadhan kutokana na uchezaji.

“Najivunia na kufurahia kuwa Muislamu. Siku moja nitatekeleza ibada ya Hijjah ambayo tunatakiwa kutimiza angalau mara moja maishani na hilo ndilo lengo langu kuu.”

ConversionConversion EmoticonEmoticon