Mazoezi ya kijeshi kati ya kenya na Jodarn,Rais na Mfalme ndani kushuhudia

Mfalme Abdullah II akiteta jambo kabla ya kuanza kwa mazoezi ya kijeshi
NAIROBI KENYA: Mfalme Abdullah wa II  wa nchi ya Jordan leo amewasili nchini Kenya na kupokelewa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta kwenye Uwanja wa ndege wa Jomo Kenyetta.
Baada ya kuwasili nchini humo mfalme huyo ameshuhudia utiaji saini wa mkataba wa kusaidiana kijeshi kati ya mataifa hayo mawili ambapo watakuwa wakibadilishana ujuzi kuhusu namna ya kupambana na suala la ugaidi kwenye nchi zao.
Majeshi ya KDF na Royal Jordanian Armed Forces kwa pamoja yamefanya mazoezi na kushuhudiwa na viongozi hao kwenye eneo la mazoezi ya kijsehi ya KDF.
Nchi zote mbili zimekumbana na matukio ya kigaidi miaka ya hivi karibuni na kupitia mkataba huu mataifa hayo yamekubaliana kwa pamoja kusaidiana kupambana na masuala ya kigaidi.
Mfalme Abdullah II amerejea nchini kwake baada ya kukamilika kwa mazungumzo hayo.


…Akiteta jambo na mwenyeji wake Rais Kenyatta.
Mfalme wa Jordan, King Abdullah wa II akisalimiana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta mapema leo


…wakishuhudia mazoezi hayo ya kijeshi.

Viongozi hao wakiteta jambo huku mazoezi ya kijeshi yakiendelea.

…mazoezi ya kijeshi yakiendelea.

Mfalme Abdullah II akizungumza na wanajeshi kwenye hafla hiyo.

Helikopta ya kijeshi ikiwa katika mazoezi hayo pia

Kiongozi wa ngazi za juu wa KDF akizungumza mbele ya Mfalme Abdullah II.


Previous
Next Post »

Ads