Ofisi ya mkuu wa mkoa mjini magharib imekataza rasimi mtu yoyote katika maeneo yoyote kufanya kazi ya omba omba
katika mkoa wa mjini magharib hali inayosababisha kuondoa haiba ya muonekano wa Nchi
hasa kwa wageni.
Akizungumza na maafisa kutoka ofisi ya mkurugenzi wa
mashataka pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama huko ofisi kwake Vuga amesema
katika mkoa huo kumekithiri vitendo vya omba omba vinavyofanywa na watu wa rika
tafauti wakiwemo wazee vijana na watoto katika maeneo mabilimbali yakiwemo
madukani, maofsini na mitaani.
Akilitolea ufumbuzi suala la uzuzuraji wa wanyama
wakiwemo ngombe, punda na wengineo ambao lilipigiwa marufuku hivi karibuni katika maeneo ya mjini na baadhi ya maeneo ya magharib amesema
Ayoub amesema
katika kuhakikisha omba omba wanaondoka katika mkoa huo
tayari mikakati imeshakamilika kutoka vyombo vya ulinzi na usalama.
Akizungumza na mbwanajr blog mmoja ya omba omba hao
hakutaka jinalake kutajwa katika mtandao huu wa
habari amesema ameamua kujiingiza katika kazi hiyo kutokana na
hali ngumu ya kimaisha.
Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara wamesema
wanasikitishwa na kazi hiyo inayofanywa na baadhi ya watu kwa kupita madukani
pamoja na kufanya makazi yao katika maeneo ya madukani hali inayopelekea kero
katika maeneo hayo.
Mmoja wa wafanyabiashara hao Said Salehe
mfanyabiasha wa bidhaa za ujasiriamali hivyo ameishauri serikali kuandaa mbinu
mbadala za kiwasaidia zitakazowezesha kuondoakana na tabia hiyo
ConversionConversion EmoticonEmoticon