Wanafunzi
wa vyuo vikuu wamehimizwa kutumia taaluma zao katika kubuni mbinu za kujiajiri
kwa lengo la kujikwamua na umaskini na
kuondokana na utegemezi wa ajira serikalini.
Akifunga
mafunzo ya siku mbili kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali juu ya utengezeji wa
picha mitandaoni muhadhir kutoka chuo cha Abdul rahman sumait Mohammed Saleh
Muhammed amesema wanafunzi wa vyuo wakiitumia ipasavyo elimu walionayo itasaidi
kuleta maendeo ya kiuchumi.
Aidha amesema baadhi ya wanafunzi wamekuwa
wakikaamitaani baada masomo yao ya vyuo na ya mafunzo walioyapata jambo ambalo
husababisha kushindwa kutimiza malengo yao na kupelekea wimbi kubwa la vijana
wasiokuwa na ajira.
Wakizungumza na zenj fm radio nnje ya mafunzo
hayo baadhi ya wanafunzi wametowa wito kwa wanafunzi wenzao kuyatumia ipasavyo
mafuzo waliyapata kwa lengo la kukuza taaluma yao katika kuimarisha uchumi na maendeleo
ya Nchini.
Zaidi ya wananfunzi 50 kutoka vyuo
mbalimbali vya Zanzibar ikiwemo Suna,Ipa,Zifa na Ispc yenye lengo la kuwaandaa
wanafunzi wa vyuo kubuni mbinu za kujiajiri wanapo maliza masomo.
ConversionConversion EmoticonEmoticon