Wachezaji wa klabu ya Manchester United, Juan Mata na Ashley Young washangaa chachacha

Wachezaji wa klabu ya Manchester United, Juan Mata na Ashley Young wamejikuta wakivishangaa viatu vya beki wa kati wa Man United Eric Bailly, ambavyo kwa huku bongo hivyo viatu tunaviita “Chachacha”, Mata na Young walivikuta viatu hivyo katika uwanja wa mazoezi wa Man united ndipo wakaamua kuviweka katika mitandao ya kijamii kwa utani.
eric
397ba27d00000578-0-image-a-32_1476786977060
Juan Mata na Ashley Young wakaona ngoja watumie kurasa zao za Instagram kumtania Eric Bailly kutokana na viatu hivyo jinsi vilivyo.
erick
young
Chachacha ni viatu flani hivi vya Plastiki ambavyo vilikuwa maarufu sana miaka ya nyuma, Zamani ulikuwa ikivaa “Chachacha” basi unaonekana wewe kwenu mambo safi, lakini baadae viatu hivyo vikashuka thamani na kuonekana kuvaliwa na watu wa hali ya chini viatu ivyo ambavyo ikivaa wakati wa jua kama unamoyo wa uvumilivu unaweza kuvivua mana huwa vinapata moto hatari.
Previous
Next Post »

Ads