Umeonesha makalio tu’, Pipi azitaja comments kwenye video ya Hafai zilizomvunja moyo

Mashabiki wanaweza kuwa na maneno ya kumpa furaha na nguvu msanii ya kufanya vizuri zaidi lakini wakati mwingine huwa na maneno makali yanayokatisha tamaa.



















Pipi ni mmoja wa wahanga wa comments za kukatisha tamaa alizozipata kwenye video ya wimbo wake ‘Hafai’ aliomshirikisha Nick wa Pili.
“Kuna mtu kwenye video alicomment akasema kwamba ‘video yako utaangalia mwenyewe, sijaona chochote zaidi ya makali tu.’ Halafu nikacheka, I was like ‘kweli yaani mimi nimeonesha makalio katika video?’ Sababu unajua sometimes mtu anakuwa anafanya kitu sio kwamba anashindwa. Yaani nina uwezo wa kufanya kama hivyo wanavyotaka nifanye, lakini kwa bahati mbaya hii ni sanaa yangu na mimi ndio ninachagua ninachotaka kukionesha kwa watu..
“Kwahiyo hiyo ni moja ya comments ambayo iliniudhi sana kwamba nikasema katika video zote za watu ukaona video yangu naonesha makalio wakati nimevaa nimejistiri mpaka watu wengine wanasema kwamba ‘kwanini umejistiri sana, kuwa modern kidogo.’
Pipi anasema aliamua kutumia video yake kuonesha ‘expressions’ zake.
Previous
Next Post »

Ads