TAARIFA KUTOKA OFISI YA MBUNGE JIMBO LA MIKUMI


 
Kupitia Taasisi yetu ya PROFESSOR JAY FOUNDATION tumefanikiwa kukabidhi WHEELCHAIR Kwa familia ya kijana ALLY MKINGI (23) ya kijiji cha KIFINGA kata ya RUAHA ambaye June mwaka 2014 aligongwa na gari la Polisi lililokuwa linaikwepa pikipiki iliyoingia ghafla barabarani, likaacha njia na kupinduka mara kadhaa na kumkuta kijana huyu aliyekuwa kando kabisa ya barabara akitembea kwa miguu.
  Ally ameumia sana na kupooza kuanzia kifuani mpaka chini na bahati mbaya sana kukosa uwezo na msaada Zaidi alikuwa amelala ndani tu kwa zaidi ya miaka 2 na mwili wake ukaanza kuharibika vibaya kwa vidonda vikubwa, Pamoja na jitihada zetu kubwa za kumtibia lakini ripoti ya madaktari bingwa wa Hospitali ya Muhimbili (MOI)wametuambia ALLY hataweza kurudi kwenye hali yake ya kawaida kwani muda umepita sana hivyo tuendelee kumtibia vidonda hivyo lakini pia wakatuambia vidonda hivyo vimesababishwa na kulala sana ndani na kujisaidia hapohapo kwa kutumia mipira hivyo kutengeneza unyevunyevu na wakatuambia ni vema tumnunulie wheelchair ili aweze kufanya mazoezi na pia kupata hewa ya nje mara kwa mara huku tukiendelea kumtibia na ndicho tunachokitekeleza..
  Kijana Ally mwenye Mke na Mtoto mmoja amefurahi sana na sasa angalau anaweza kuonana na marafiki zake wa zamani ambao wengi hajaonana nao kwa muda mrefu lakini pia inampunguzia sana upweke aliokuwa nao wa kukaa ndani Peke yake bila kuwa na uhakika wa kesho yake. ..
Mungu ni mwema sana na tunamtumaini yeye tu ili aweze kurudisha furaha na faraja kwa kijana huyu anayeteseka sana na familia yake.
Pichani Ally na Mama yake mzazi na kaka yake mkubwa Abdalla ambaye ndie anamuhudumia kwa kila kitu wakiwa na Mbunge wa MIKUMI nje ya nyumba yao!!

Imetolewa na:~
Ofisi Ya Mbunge
Mikumi
22/10/2016
Previous
Next Post »

Ads