Son Hueng-Min na Jurgen Klopp wameshinda tuzo ya EPL ya mwezi Septemba

Mchezaji wa klabu ya Tottenham Hotspur Son Hueng-Min ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa EPL mwezi Septemba akiwashinda Kevin De Bruyne,Theo Walcott,Romelu Lukaku na Adam Lallana waliokuwa wakiwania tuzo hiyo.

Son anakuwa ni mchezaji wa kwanza kutoka barani Asia kuchukua Tuzo hiyo.
Mchezaji huyo kutoka Korea Kusini, amesaidia timu yake kushinda mechi zote 3 za mwezi huo, katika mwezi Septemba kunako ligi hiyo amecheza mechi 3, amefunga magoli manne, Assist 1.
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp nayeye ameshinda Tuzo ya kocha Bora wa EPL mwezi Septemba akiwabwaga Pep Guardiola,Alan Pardew,Arsene Wenger na Maurcio Pochettino waliokuwepo katika kinyang’airo hicho.

Previous
Next Post »

Ads