Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein ametaka kuwajibishwa watendaji wa serikali waliowaingiza wazee wasiokuwa na sifa kwenye orodha ya malipo ya pencheni.
Akizungumza katika maadhimisho ya siku ya wazee duniani uwanja wa Gombani Pemba ameitaka Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto kuwatafuta watumishi hao na kuwajibisha.
Amesema anazo taarifa ya kuwepo baadhi ya wazee waliorozeshwa kwenye urodha ya malipo hawajatimiza miaka 70 jambo ambalo linakwenda na utaratibu uliokusudiwa.
Dk. Shein pia amesema amesema wazee wenye sifa waliostahili kuingizwa kwenye daftari la malipo lakini hawakupewa fursa hiyo na kuiagiza Wizara hiyo kuwatambua watu hao.
Wakizungumza na mwandishi wetu nje ya madhimisho hayo baadhi ya wameiomba serikali kundaa utaratibu wa kuwapatia huduma za afya na matibabu kutokana na wengi wao hawana uwezo.
Madhimisho ya Siku ya Wazee Duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 1 Oktoba kila mwaka, na kwa Zanzibar mwaka huu maadhimisho hayo yamefanyika kisiwani Pemba.









ConversionConversion EmoticonEmoticon