Rais JPM Atengua Uteuzi wa Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, Tanga


Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Rais Dk. John Pombe Magufuli leo ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga Mkoani Tanga, Emmanuel Mkumbo.
Bwana Mkumbo alikuwa anakabiliwa na tuhuma za kujifanya ofisa wa usalama wa taifa nakumtishia kwa bastola askari wa usalama barabarani wakati wakielekea kituo kidogo cha polisi Kingoluwira, Morogoro alikotaka apelekwe kuzungumza na mkuu wa kituo baada ya kukamatwa akiwa amezidisha Mwendo kasi katika barabara kuu ya Morogoro – Dar es Salaam.
jpm-atengua
Previous
Next Post »

Ads