Neymar kusaini mkataba mpya wa Barcelona Ijumaa hii

Klabu ya Barcelona imethibitisha kuwa Neymar atasaini mkataba mpya Ijumaa hii ambao utambakisha kwenye timu hiyo mpaka Juni 2021.

Kupitia mtandao wa Twitter wa timu hiyo, wameandika, “[CONTRACT NEWS] @neymarjr will sign new contract on Friday that will keep him at the Club until June 2021.”
Mkataba huo mpya wa Neymar unadaiwa kuwa utamfanya awe analipwa mshahara mkubwa zaidi tofauti na anaopokea sasa wa £230,000 kwa wiki na atarajiwa kumzidi Lionel Messi ambaye anapokea kiasi cha £256,000 kwa wiki.
Endapo Neymar atasaini mkataba huo atakuwa amezima ndoto za timu ya PSG ya Ufaransa iliyokuwa ikimuwania kwa muda mrefu huku ikiwa tayari kutoa kiasi cha paundi milioni 200 kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo aliyekuwa anawindwa na Manchester United.
Neymar amefanikiwa kutengeneza ushirikiano mzuri kwenye nafasi ya ushambuliaji ya Barcelona akishirikiana na Messi pamoja na Luis Suarez na kufanikiwa kuifungia timu hiyo jumla ya mabao 77 tangu alipojiunga na timu hiyo misimu mitatu iliyopita huku wote watatu wakifanikiwa kufunga jumla ya mabao 276.
Previous
Next Post »

Ads