HOSPITALI ya Taifa Muhimbili imepokea msaada wa kifaa maalumu cha kusaidia kuimarisha utendaji wa misuli (training balance and coordination). Msaada huo umekabidhiwa na Profesa Henrik Hautop Lund kutoka Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Denmark Copenhagen.
Profesa Henrik amesema Fiziotherapia Utengamao ni moja ya matibabu ya misuli iliyoathiriwa na magonjwa yaliyoathiri ubongo kutokana na kiharusi au mtindio wa ubongo kutokana na majeruhi wakati wa kuzaliwa.
Profesa Henrik amekuwa na ushirikiano wa kiutafiti wa utengamao na Dk Khadija Malima ambaye ni Mtafiti Kiongozi ( Afya) kutoka Tume ya Sayansi na Teknolojia. Utafiti huo unahusu vifaa (Tiles) vya teknolojia ambayo hutumika kutibu misuli, mwendo na kuchangamsha akili kwa watoto wenye mtindio wa ubongo wa kiasi.“Vifaa hivi humwezesha mgonjwa kufanya mazoezi na pia kufurahia kama mchezo, hivyo wateja wanufaika ni wale wenye kiharusi waliopata ajali na hawawezi kutembea, lakini wanahitaji kuimarisha misuli.
“Lengo ni kufanya utafiti utakaothibitisha faida ya teknolojia hii ili kusambaza huduma ya matibabu ya utengamao sehemu zote nchini hata kwenye jamii kwani teknolojia hii inatumia betri kuchaji na inakaa saa 20,” amesema Dk Malima.
Pia teknolojia hiyo imetolewa katika Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali la Inuka Rehabilstiona centre.
Source: MNH
ConversionConversion EmoticonEmoticon