Bado jina la Wayne Rooney linazidi kutawala katika social network, ikiwa saa chache tu zimepita toka mkewe Coleen Rooney aandike kuoneshwa kusikitishwa kwake kupitia account yake ya twitter kutokana na tukio la weekend kuzomewa kwa mumewe Wayne Rooney katika mchezo wa England dhidi ya Malta.
Mashabiki waliokuwa wamejitokeza katika uwanja wa Wembley walimzomea Wayne Rooney katika mchezo huo uliomalizika kwa England kuondoka na ushindi wa goli 2-0, nahodha wa zamani wa Chelsea John Terry ni moja kati ya watu ambao hawakufurahishwa na kitendo kile na ametumia ukurasa wake wa instagram kuoneshwa kusikitishwa kwake.
“Rooney mfungaji bora wa England wa muda wote katika historia na hivi karibuni atakuwa moja kati ya manahodha bora waliowahi kuiongoza England, moja kati ya wachezaji bora ambao nimewahi kuwaona na furaha kucheza pamoja nao, bado ni LEGEND wa Everton, Man United, England na dunia ya mpira kwa ujumla, anatakiwa kuheshimiwa sana huyu mtu” nae mke wa mchezaji huyo alisema hivi
Coleen Rooney, mke wa nahodha wa Manchester United na England Wayne Rooney, amewashutumu wanaomkosea mumewe akisema sasa wamezidi.
Amewataka "kufyata ndimi zao" na kusema kwamba wao ni binadamu hawajaungwa kwa plastiki.
"Sisi hatujaundwa kwa plastiki, yeye si wa plastiki, sisi ni binadamu," amesema.
Nahodha huyo wa England alizomewa na mashabiki mechi ambayo England walilaza Malta Jumamosi.
Amewekwa kwenye benchi mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia itakayochezwa Jumanne dhidi ya Slovenia.
Mashabiki wengi sasa wanasema huenda muda umefika kwa Rooney kustaafu soka ya kimataifa.
Lakini Coleen amekerwa nao na kusema: "Nipanda sana vile kila mtu ana maoni yake. Tulieni, twacheni. Baadhi wanasahau kwamba watu wengine wana hisia pia."
Lakini wengine wanasema wana haki ya kuzungumzia uchezaji wa Rooney kwa sababu analipwa pesa nyingi.
Coleen amesema ukosoaji ambao umeelekezwa kwa mumewe unawaathiri watoto wao pia.
Wayne Rooney alichezea taifa lake mechi ya 117 dhidi ya Malta. Amefunga bao moja pekee katika mechi 12 za majuzi zaidi alizochezea taifa lake na klabu yake msimu huu.
ConversionConversion EmoticonEmoticon