Cassper Nyovest amuumbua Kanye West kwenye hili

Wiki hii Kanye West amelalamika kuwa rappers wengine wamekuwa wakimuiga katika namna navyopangalia show zake, ikiwemo kuwa na jukwaa linaloelewa hewani.
Wakati akitumbuiza kwenye show yake huko Edmonton, Kanye alisikika akisema: “This the original! Accept no imitations!” Akiwa kwenye stage hiyo inayoelea, Kanye aliwashutumu wasanii wenzake kwa kumuiga.
Hakumjata mtu lakini Drake pia amekuwa akitumia jukwaa kama hilo kwenye show zake. Sasa sakata hilo halijaishia Marekani tu. Blogger maarufu aitwaye Dj Akademics, aliweka picha ya show ya mwaka jana ya Cassper Nyovest, Fill Up The Dome kwenye Instagram na kuandika:
#kanyewest might be talking about this guy when he said “they stealing our stages” …. did anyone do floating stages before Kanye or did he invent it?
Cassper alimjibu Akademics:
Academics naye aliandika: So #kanyewest accused people of stealing his stage idea. Come to find out his current stage idea has already been done by a African artist last year .. so it would be more likely Kanye stole rather than #casspernyovest.
Kufuatia majibizano hayo, blog nyingi za Marekani zimemtaja Cassper kama msanii aliyetumbuiza kwanza kwa jukwaa linaloelea.

Previous
Next Post »

Ads