Mkuu wa Mkoa hawaimiza wananchi kuwekeza Morogoro


SERIKALI ya Mkoa wa Morogoro imesema kuwa haitosita kumchukulia hatua kali za Kisheria mtendaji itakae bainika kumkwamisha mtu mwenye nia ya kuwekeza katika mkoa huo

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dakta Kebwe Steven Kebwe wakati akizungumza kuhusu fursa za uwekezaji katika Mkoani humo

Dakta Kebwe amesema   wawekezaji wanatakiwa kufuata tararibu ziliwekwa na serikali katika eneo hilo na endapo watakutana na urasimu wanatakiwa kuwasilisha malalamiko yao kwake ili mtendaji huyo aweze kuchukuliwa hatua.
Maporomoko ya maji ndani ya milima ya Uluguru, Morogoro

Aidha amesema kuwa Mkoa wa Morogoro kunapatika fursa mbalimbali katika uwekezaji wa Kilimo ufugaji utalii na kuwataka fursa hizo zitumike kwa watu wote na kuachana na dhana kuwa mwekezaji lazima atoke nje ya nchi

Mkoa wa Morogoro ni mkoa wenye vivutio mbalimbali ikwemo uoto wa asili mabonde mazuri kwaajili ya kilimo mbuga za wanyama hali iliyofanya Mkoa huo kuandaa mkutano maalum wa siku mbili kwaajili ya kutangaza fursa hizo.
Previous
Next Post »

Ads