Zanzibar>Uchumi wapanda to 4.5 hadi....Soma zaid

 
Waziri wa  Nchi ofisi ya Makamo wa pili wa Rais amesema hali ya ukuwaji wa uchumi umekuwa kwa kutoka asilimia 4.5 hadi kufikia asilimia 7 kutokana na wananchi kutoa ushirikiano wa kujiunga na shughuli za kimaendelo.

   Akizungumza na waandishi wa habari huko ofisini kwake vuga kuhusu mafanikia yalofikiwa katika ofisi hiyo  ndani ya kipindi cha uongozi wa awamu ya saba amesema hali ya uchumi imekuwa  katika sekta mbalimbali ikiwemo  Bandari ,Viwanja vya ndege,Afya na miundombinu ya Barabara.

   Hata hivyo amesema katika ukusanyaji wa mapato kwa wananchi pato la mwananchi limekuwa kwa zaidi ya dola mia tisa ambapo awali ilikuwa ni dola mia 6 jambo ambalo limechangia kukuwa kwa harakati za uchumi zilizopo licha ya matatizo ya kisiasa yanayojitokeza 
.
   Akizungumzia suala la mradi wa kusaidia kaya maskini TASAFF amefahamisha kuwa  mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa katika kuinua shughuli za kimaendeleo katika kuboresha  Elimu na miundombinu ya Barabara hapa Zanzibar ambapo takriban  billioni 5 zimetumika kusaidia kaya 36 elfu 42 katika shehia za unguja na pemba.

    Aidha ametowa wito kwa wananchi kuacha  tofauti za kisiasa zitazopelekea  kudumaza maendelo ya nchi badala yake waimarisha ushirikiano katika kukuza  maendelo ya kiuchumi  kwa lengo la kujikwamua na hali ya umaskini . 
Previous
Next Post »

Ads