Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imeahidi
kuyapatia ufumbuzi matatizo yanayoikumba
sekta ya elimu ikiwemo tatizo la kuchelewa kulipwa madeni yao ndani ya kipindi
cha miezi kumi ijayo.
Akizungumza katika kilele cha siku ya
maadhimisho ya walimu duniani Naibu Waziri wa elimu na mafunzo ya amali
Zanzibar Mmanga Mjengo Mjawiri amesema serikali inatambua matatizo yote yanayo ikabili sekta ya elimu
na kuwataka walimu kuwa na uvumilivu wakati matatizo hayo yapo katika
hatua ya kupatiwa fumbuzi.
Hata hivyo amesema mbali na walimu
kukabiliwa na matatizo mbalimbali wanapokuwa kazini ikiwemo ukosefu wa nyenzo
za kutosha katika kutoa elimu kwa wananfunzi lakini wasivunjike moyo badala
yake wafuate maadili ya kazi zao ili kuinuwa kiwango cha ufaulu kwa wanafunzi.
Wakati huo huo Raisi wa Chama cha walimu
Zanzibar ZATU Seif Muhammed Seif ametowa wito kwa serikali kuandaa Tume ya
walimu itakayo wasaidia kutatua matatizo yanayowakabili kwa wakati .
Awali akisoma risala kwa ya chama cha walimu
Zanzibar ZATU katibu mkuu wa chama hicho Mussa Omar Tafur amefahamisha kuwa
mbali na kufanya kwa kufauta maadili ya kazi zao lakini wanarejeshwa nyuma na
matatizo yanayowakabiuli kwa muda mrefu ikiwemo uwiyano mbovu wa mishahara usiozingatia
elimu zao.
Siku
ya walimu duniani huadhimishwa kila ifikapo octobar5 ya kila mwaka ambapo kwa
mwaka huu ikiwa na ujumbe usemao ‘’tuwathamini walimu kuinua hadhi yao’.
ConversionConversion EmoticonEmoticon