Kocha mkuu wa klabu ya Monaco Leonardo Jardim amesema streka Radamel
Falcao atakuwepo katika mtanange kuwakabili Toulouse fc ijumaa hii kama vipimo
vitaenda vizuri.
Falcao hajacheza mechi yoyote tangu apate
mtikisiko katika ligi ya Ufaransa septemba 21 lakini amekuwa akipata mazoezi
katika kipindi hiki.Kocha wake ameendelea kusema kuwa kama atafanikiwa kwenye
vipimo hivyo jumatano hii atakuwa katika orodha ya kuikabili timu hiyo ya
Toulouse fc.
Wakati huo
huo mchezaji streka huyo raia wa Colombia mwenye umri wa miaka 30 ambae katika
msimu huu ameona nyavu mara 3 ndani ya mechi sita,kocha huyo amesema taendelea
kuwa chaguo lake namba moja katika timu hiyo.
Falcao
alijiunga na Monaco mwezi wa tano 2013 akitokea Atletico Madrid kwa dili
lilowagharimu paundi milioni €60 sawa na dolar million ($67 million),na alikaa nje ya
uwanja baada ya kupata maumivu ya goti 2014 kwenye kombe la dunia.
ConversionConversion EmoticonEmoticon