Muigizaji mashuhuri, aliyepigwa marufuku katika sekta ya uigizaji ya Hausa kutokanana 'utovu wa nidhamu' ameomba radhi.

Bi Sadau ameomba radhi kwa aliowaudhi, lakini amesema 'hakufanya makosa'.
Filamu za Hausa ni maarufu sana kaskazini mwa Nigeria kuliko na idadi kubwa ya waislamu ambako ni mwiko kwa wanaume na wanawake kushikana mikono hadharani.
Sekta hiyo , inayojulikana kama Kannywood, imeshutumiwa na viongozi wahafidhina wa kidini kwa kuharibu maadili ya watu.

Filamu za KannywoodImage copyright

Muungano wa filamu Motion Pictures Practitioners nchini Nigeria ulimpiga marufuku muigizaji huyo katika filamu za Kannywood, ukisema kuwa kuonekana kwake katika video hiyo kunakwenda kinyume na maadili ya sekta hiyo ya uigizaji.
Uliongeza kuwa unatumai kuwa marufuku hiyo itakuwa funzo kwa waigizaji wengine wanaotarajiwa kuwa 'vioo vya jamii'.
Bi Sadau anasema yeye ndio wa kulaumiwa kwa kilichotokea lakini amelalamika kuwa katika kazi yake, hana budi "kuwagusa watu pasi kuwana dhamira mbaya ".
Lakini amewahakikishia watu kuwa atakuwana nidhamu zaidi akiongeza kuwa: "nina mipaka ambayo siwezi kuthubuti kuyavuka."

Rahma Sadau na ClassiqImage copyright
Rahma Sadau na ClassiqImage copyright

Muigizaji nyota huyo wa Kannywood alionekana katikavideo ya wimbo wa Classiq kwa jina 'I Love You'.
Classiq anaonekana kulemazwa kwa mapenzi na mchuuzi wa mboga sokoni amabye ni Bi Sadau.
Mwanzo anamkataa na anamfukuza lakini mwishowe anamkubali.
Wanashikana mikono na kukumbatiana kidogo, jambo ambalo ni kawaida katika filamu za matifa ya magharibi.
Lakini kwa wengi kaskazini mwa Nigeria wameona kwamba amevuka mpaka na Classiq katika video hiyo,
Previous
Next Post »

Ads