Manchester united yatoka sare nyumbani

Klabu ya Manchester United imelazimishwa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Stoke City katika mechi ambayo Manchester United iliotawala mchezo kwa kipindi cha mda mrefu.
Baada ya kipa wa Stoke kuokoa mashambulio mengi katika kipindi cha kwanza cha mechi,United ilijiweka kifua mbele baada ya mchezaji wa ziada Anthony Martial kufunga bao la kwanza.
Ilikuwa pigo kubwa kwa Stoke ambayo ilikuwa haijafanya shambulio lolote katika ngome ya United.
Lakini baada ya Jon Walters kupiga krosi, Allen alifika na kusawazisha hivyo basi kufuinga midomo ya mashabiki wa United ambao walikuwa wakiimba katika kipindi chote cha mchuano huo.
Stoke City ambayo iko katika nafasi ya pili kutoka mwisho sasa imejiongezea matumaini ya kuondoka katika eneo la mkia la ligi hiyo ya Uingereza.

Previous
Next Post »

Ads