kikao cha wadau wa maendeleo juu ya kuangalia maendeleo ya TASAF

Katibu mkuu Ofisi ya makamo wa Pili wa rais Joseph Meza akiapishwa

Katibu mkuu Ofisi ya makamo wa Pili wa rais Joseph Meza amesema katika kukabiliana na umaskini watendaji wanaosimamia miradi ya kayamaskini katika shehia wanajukumu la kukusanya taarifa zilizosahihi ili miradi hiyo kuwafikia walengwa.
    Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha wadau wa maendeleo juu ya kuangalia maendeleo ya TASAF amesema mbali na serikali kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwatafutia maendeleo wananchi walio wanyonge lakini wanarejeshwa nyuma kutokana na baadhi ya viongozi wa shehia kufanyakazi kinyume na utaratibu iliowekwa.
    Hata hivyo amefahamisha kuwa ili kukabiliana na hali ya umaskini nchi jamii haina budi kuimarisha ushirikiano katika kuondowa matatizo yanayowakabili kaya maskini kwa lengo la kukuza miradi ya maendeleo inayotolewa.
    Wakati huo huo akizungumzia maendeleo ya TASSAF kwa kwa ujumla Mkurugenzi mtendaji wa mfuko wa maendeleo wa kusaidia kaya maskini TASAF Ladis laus Mwanaya ameafahamisha kuwa TASSAF ya awamu ya tatu imewanufaisha wananchi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu na afya na kupelekea ongezeko la miradi ya kimaendeleo nchini.


    Zaidi ya billin mia tatu wamepatiwa walengwa katika kusaidia kaya amaskini juu ya kusaidi miradi mbali mbali katika jamiii.
Previous
Next Post »

Ads