Ni vigumu kumpata mwanaume wa umri wa miaka zaidi ya 20 akiwa bado ni bikira
-Hata hivyo, kuna mwanaume mmoja aliye na miaka 31 ameushangaza ulimwengu kwa ‘kujihifadhi’ kwa mke wake wa usoni
Suala la ubikira ni limejaa utata. Jamii inapenda kusisitiza mwanamke kuwa bkira hadi atakapoolewa.
Habari Nyingine: Nairobi ni kati ya miji mikuu yenye vipusa warembo zaidi Afrika
Kwa upande mwengine, wanaume wanatiwa motisha kujaribu iwapo ‘chombo chao kinafanya.’
Ni nadra sana kumpata mwanaume aliyekomaa akiwa bikira kwani tukio kama hilo litahusishwa na kasoro ya maumbile.
Hata hivyo, jamaa mmoja mwenye umri wa miaka 31 ameapa kutunza bikira yake hadi atakapooa.
Jim Dre Westbrook ni Mwamerika ambaye hajawahi kushiriki ngono tangu azaliwe.
JimDre Westbrook. Westbrook haoni haya kutangaza uamuzi wake wa kuwa bikira hadi atakapooa. |
Linalowashangaza wengi ni kuwa jamaa huyu hana kasoro yoyote ya kimwili. Yeye ameamua kujitunza hadi siku atakapooa.
Tena hayaishii hapo jamaa huyu ni mwenyeji wa Las Vegas, mji maarufu kwa anasa.
Westbrook haoni haya kutangaza uamuzi wake. Yeye ni mcha Mungu na anaamini uamuzi wake wa kutoshiriki ngono hadi ndoa unafaa.
ConversionConversion EmoticonEmoticon