MATOKEO YA UTAFITI WA MAPATO NA MATUMIZI YA KAYA BINAFSI YAFANYIKA ZANZIBAR.

Waziri wa fedha na ,mipango Zanzibar Dk,Khalid Salum Muhammed amesema ili kupambana na hali ya umaskini  iliopo katika kisiwa cha Zanzibar  wizara za serikali na taasisis binafsi zina wajibu wa kutunza takwimu za maendeleo nchini.
   Akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya matokeo ya utafiti wa mapato na matumizi ya kaya amesema hali ya umaskini bado imeshika kasi katika sehemu mbalimbali ikiwemo Zanzibar hususani vijijini  hivyo ni vyema kwa tasisi kujuwa umuhimu wa kutunza takwimu ili kuinua uchumi wan chi.
   Aidha ametowa wito kwa wafanya kazi wa taasisi hizo kuwa na ushirikiano katika ukushanyaji  takuwimu muhimu ili kujua matatizo yaliyopo katika jamii kwa lengo la kuondokana na utegemezi na kuweza kubuni njia za kukuza maendeleo
   Kwa upande wake mtakwimu mkuu kutoka ofisi ya mtakwimu Zanzibar Mayasa mahfoudh mwinyi amefahamisha kuwa lengo la kuwepo kwa ripoti hiyo ni kukusanya taarifa na uchambuzi utakao rahisisha kutowa hudumu muhimu katika jamii ili kupunguza umaskini.

 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk,Khalid Salum Mohammed wamwanzo kushoto akionesha kitabu cha Uzinduzi wa  Matokeo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2014/15 uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Yubu Mohd Mahamoud na mwengine ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya zanzibar Mayasa Mahfoudha Mwinyi.
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk,Khalid Salum Mohammed akimkabidhi Muakilishi wa UNICEF Francesca Morandini kitabu cha  Matokeo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2014/15 uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. 

 Baadhi ya Waalikwa waliohudhuria katika Uzinduzi
 Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mayasa Mahfoudha Mwinyi akitoa maelezo kuhusu utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya binafsi wa Mwaka 2014/15 katika Uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 Muakilishi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Zanzibar Anna Senga akitoa maelezo kuhusu  utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya binafsi wa Mwaka 2014/15 katika Uzinduzi uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar.
 Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohd Mahmoud

 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk,Khalid Salum Mohammed 
 Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Dk,Khalid Salum Mohammed wamwanzo kushoto akizindua Matokeo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi wa Mwaka 2014/15 uliofanyika katika Ukumbi wa Sanaa Rahaleo Zanzibar. katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Yubu Mohd Mahamoud na mwengine ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya zanzibar Mayasa Mahfoudha Mwinyi.

Previous
Next Post »

Ads